1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jengo la poromoka na kuuwa watu Misri

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfru

ALEXANDRIA:

Kwa uchache watu watano wameuawa baada ya jengo la orofa 12 kuporomoka katika mji wa Misri wa Alexandria.

Afisa mmoja, ambae hakutaka kujitambulisha, amesema kuwa watu wengine baado inaaminiwa wamenaswa katika vifusi vya jengo hilo.

Polisi inasema kuwa jengo hilo, la miaka 30, mwanzo lilikuwa la orofa 5 lakini orofa zingine tano zikaongezwa hapo baadae.Visa vya nyumba kuporomoka vimekuwa vikitokea mara kwa mara nchini Misri.

Majengo mengi nchini humo hujengwa kiholela na bila kuruhusiwa na wahusika.