1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JENIN: Wapalestina waandamana kufuatia kifo cha Saddam

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeS

Wapalestina takriban 1,000 wameandamana hii leo mjini Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan kufuatia kunyongwa kwa rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein.

Wakiwa wamebeba jeneza tupu na picha za Saddam, waandamanaji hao walipiga kelele wakiilaani Iran, Marekani na Israel katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wafuasi wa waastani wa chama cha Fatah cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Hapo jana wapalestina 200 waliandamana mjini Bethlehem kupinga kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Kiongozi huyo alikuwa maarufu miongoni mwa wapalestina kwa kuzilipa jamii za washambuliaji wa kujitoa muhanga maisha na wapiganaji dhidi ya Israel, pamoja na mashambulio ya makombora dhidi ya Israel wakati wa vita vya Ghuba mnamo mwaka wa 1991.