1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Abbas na Olmert kujadili mgogoro wa Mashariki ya Kati

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpQ

Wajumbe wa kundi la kidiplomasia la pande nne, kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati,watakutana mjini Jerusalem,Jumanne ijayo kujadili matokeo ya hivi karibuni katika kanda hiyo.Kundi hilo linafungamanisha Marekani,Urusi,Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.Mbali na mkutano huo,siku ya Jumatatu vile vile,Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert na Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas watakutana katika mji wa kitalii wa Sharm-el-Sheikh nchini Misri.Mkutano huo utajadili mzozo wa sasa katika maeneo ya Kipalestina na utahudhuriwa pia na Rais Hosni Mubarak wa Misri na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan.Huo utakuwa mkutano wa kwanza kati ya Olmert na Abbas,tangu kundi la Kipalestina la Hamas,kuvitimua vikosi vya chama cha Fatah cha Abbas na kudhibiti eneo zima la Ukanda wa Gaza.