1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Barak ashinda uchaguzi wa chama cha Labour

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsD

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak amemshinda mwanagenzi wa siasa Ami Ayalon katika uchaguzi uliokuwa wa mchuano mkali kuwania kukiongoza chama cha Labour.

Barak amejipatia kura 34,960 wakati Ayalom amejipatia kura 31,100 matokeo ramsi yanatazamiwa kutangazwa baadae leo hii.

Barak anatazamiwa kuziba nafasi ya kiongozi wa chama Amir Peretz aliyeondolewa madarakani katika wadhifa wa uwaziri wa ulinzi katika serikali ya Waziri Mkuu Ehud Olmert.Barak ametowa wito wa kujiuzulu kwa Olmert kutokana na kuboronga katika vita vya mwaka jana dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.

Pia amedokeza kwamba atakitowa chama chake cha Labour katika serikali ya sasa ya mseto na chama cha Kadima cha Olmert.