1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Condoleezza aanza ziara ya mashariki ya kati.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCan
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor aisusia tena mahkama ya mjini The Hague.
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor aisusia tena mahkama ya mjini The Hague.Picha: AP

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili nchini Israel, akianza ziara ya mataifa matano ya mashariki ya kati lakini amesema kuwa hana mkakati mpya wa amani .

Marekani iko katika mbinyo kutoka katika mataifa ya Ulaya na ya washirika wake wa kiarabu hivi sasa kufufua mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel chini ya kile kinachoitwa mpango wa amani wa kutayarisha njia.

Rice amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel pamoja na wa mambo ya kigeni na atamtembelea rais wa Palestina mwenye msimamo wa kati Mahmoud Abbas leo Jumapili.

Maafisa kutoka katika chama cha Abbas cha Fatah na wale wa chama hasimu cha Hams wamesema wakati huo huo kuwa hatua zimepigwa katika mazungumzo ya faragha nchini Syria katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina. Waziri mkuu Ismail Haniyah kutoka chama cha Hamas ametoa wito kwa pande zote mbili kusitisha msuguano wao wa kuwania madaraka ambao umesababisha hali ya ghasia.