1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yaanza kutoa fedha kwa Palestina

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmj

Serikali ya Israel imeanza kutoa mamilioni ya fedha za ushuru za Palestina ilizokuwa ikizizuilia. Kiasi cha euro milioni 90 zililipwa kwa serikali ya rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, hapo jana na fedha zaidi zinatarajiwa kutolewa baadaye wiki hii.

Israel inazuilia kiwango cha euro takriban milioni 400 kama ushuru wa Palestina, ambazo ilikataa kuzitoa baada ya chama cha Hamas kushinda uchaguzi uliofanyika mnamo mwezi Januari mwaka jana katika maeneo ya Wapalestina. Israel pamoja na jumuiya ya kimataifa, imeahidi kumsaidia rais Abbas kukabiliana na kundi la wanamgambo la Hamas.

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, ameahidi pia kuwaachilia huru wafungwa 250 wa kipalestina kama ishara ya urafiki kwa rais Abbas, lakini hatua hiyo bado haijatekelezwa huku maafisa wa usalama wakisubiriwa waamue wafungwa wanaotakiwa kuachiliwa huru.