1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem . Israel yagutushwa na mwelekeo mpya unaotakiwa na Marekani kuhusu mashariki ya kati.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClI

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel amewasili nchini Marekani leo huku kukiwa na wasi wasi mshirika mkubwa wa taifa hilo la Kiyahudi Marekani inabadilisha mtazamo wake baada ya ripoti inayoitaka Marekani kuongeza juhudi zake za kuleta amani katika mashariki ya kati.

Tzipi Livni anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice pamoja na maafisa wengine wakati wa ziara yake hiyo, ambayo italenga katika athari zitakazopatikana kutokana na ripoti iliyokabidhiwa kwa rais Bush na kundi lililotathmini hali nchini Iraq.Ripoti hiyo imesema kuwa maendeleo yatakayopigwa kuhusu uhusiano kati ya Waarabu na Waisrael ni muhimu kuweza kuinusuru Iraq. Wakati huo huo jumuiya ya nchi za Kiarabu imeiponda ripoti hiyo inayotaka mabadiliko katika sera za Marekani kuelekea Iraq , na kuita kuwa na kujitoa aibu, lakini imesifu wito wa kutaka kuongezwa juhudi katika kutanzua mzozo kati ya Israel na Palestina.