1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Olmert akutana na Abbas

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQx

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wamekutana mjini Jerusalem kwa mazungumzo yenye lengo la kuweka miongozo kwa ajili mkutano wa amani unaodhaminiwa na Mareakni utakaofanyika mwezi wa Novemba.

Viongozi hao walikuwa wakitazamiwa kujadili uwezekano wa kuanzishwa kwa taifa la Kipalestina litakalotambuliwa kimataifa.

Katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Israel Olmert amependekeza kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Palestina wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan.