1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Rais mpya wa Israel kuchaguliwa Juni 13

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3m

Bunge la Israel litamchagua rais mpya tarehe 13 mwezi Juni.Uamuzi huo umechukuliwa na jopo la ushauri la wabunge wa Israel.Wadhifa wa rais Moshe Katsav wa miaka saba unamalizika tarehe 15 Julai.Hivi sasa,Katsav kwa muda,yupo katika likizo ya lazima kufuatia madai kuwa aliwasumbua na kuwabaka wafanyakazi wa zamani kadhaa wa kike.