1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Waandamana kupinga ukarabati

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTY

Polisi ya Israel imetumia gesi ya kutowa machozi na risasi za mpira kutawanya waandamanaji wa Kipalestina waliokuwa wakivurumisha mawe katika msikiti wa Al Aqsa mjini Jerusalem

Takriban waandamanaji 17 na polisi 15 wamejeruhiwa katika vurugu hizo zilizozushwa kutokana na kazi za uchimbaji katika eneo takatifu la Mlima Mzeituni kama linavyojulikana na Wayahudi na kutambuliwa na Waislamu kuwa ni eneo takatifu la Haram al Sharif. Wapalestina wanasema shughuli hizo za ukarabati zinaweza kuharibu msingi wa eneo hilo la msikiti lakini maafisa wa Israel wanasisitiza kwamba kazi hiyo inahitajika ili kulinusuru eneo hilo la kale na wamehakikisha kwamba hakutakuwepo na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.

Misri,Jordan na Pakistan zimeitaka Israel kusitisha shughuli hizo za ukarabati kwenye eneo la kupandia msikitini ambazo wanaziona kuwa zinatanuwa wigo wa umwagaji damu na kuweka vikwazo katika mchakato wa amani.

Hatua hiyo ya Israel inaonekana kukiuka maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo yanataja kwamba hatua yoyote ile ya uharibifu au ya kukufuru mahala na maeneo takatifu mjini Jerusalem kunaweza kukahatarisha vibaya sana amani na usalama wa kimataifa.