1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem: Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Rice, akutana na Ehud Olmert wa Israel na Mahmud Abbas wa Palastina.-

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR1

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, yuko Jerusalem akifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert. na rais wa Wapalastina, Mahmud Abbas. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Bibi Rice alisisitza juu ya haja ya kuliunga mkono suluhisho la kuweko dola mbili, ile ya Israel na ya Wapalastina.. Lakini leo mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliopangwa kufanywa baada ya kukutana baina ya Mahmud Abbas na Bibi Rice ulifutwa bila ya kutolewa maelezo. Israel na Marekani zilikubaliana kabla ya kufanyika mkutano huu wa pande tatu kutokuwa na mawasiliano na serekali ya Wapalastina ambayo haitakana matumizi ya nguvu, haitaitambua dola ya Israel na haitoikubali mikataba iliotiwa saini hapo kabla. Mazungumzo hayo ya pande tatu yaligubikwa na majaribio ya Wapalastina ya kukamilisha kuundwa serekali yao ya Umoja wa Taifa baina ya Bwana Abbas na chama cha Kiislamu cha Hamas ambacho kinakataa kuitambua dola ya Israel.