1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Blair aanza kazi yake kama mjumbe wa mashariki ya kati

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfo

Waziri mkuu wa Uingereza wa zamani Tony Blair anaanza kazi yake kama mjumbe maalum mpya wa eneo la Mashariki ya Kati.Mazungumzo ya kutafuta amani ya eneo hilo yanaongozwa na pande nne za Marekani,Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa na Urusi.Kiongozi huyo yuko mjini Jerusalem kufanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni.Kabla ya hapo alikutana kwa muda mfupi na waziri wa mambo ya nje wa Jordan.Bwana Blair anatarajiwa kukutana pia na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert vilevile Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

''Sera ya pamoja kwa eneo la mashariki ya kati sharti ianze na Israel na Palestine.Huo ndio wito wetu…baada ya hapo sharti tutie juhudi nchini Lebanon ili kuunganisha jamii zote za KiArabu zilizo na msimamo wa wastani katika mataifa husika ili kupata amani ikiwemo Iraq.''

Hata hivyo Bwana Blair hatakutana na wawakilishi wa chama cha Hamas.Majukumu yake kama mwakilishi wa pande nne zinazojadilia amani ya mashariki ya kati hayampi madaraka ya kufikia makubaliano ya mwisho ya amani.