1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Israel kuondoka kwenye maeneo ya Ukingo wa Magharibi

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMw

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema leo kwamba Israel itaondoka kutoka kwenye sehemu kadhaa za Ukingo wa Magharibi ikiwa ni katika hatua ya mwisho ya kutafuta amani na Wapalestina.

Bwana Olmert ameyasema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice kutangaza mjini New York kuwa Marekani itaandaa mkutano na wanachama wa pande nne wanaoshughulikia mpango wa amani ya mashariki ya kati pamoja na nchi za kiarabu ikiwemo Syria mwezi Novemba.

Hata hivyo waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert akizungumzia juu ya mkutano huo wa mwezi Novemba amesema kuwa makubaliano ya amani bado yako mbali mno.