1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem:Israel yakataa pendekezo la Wapalestina.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpf

Israel imelikataa pendekezo la wapalastina la kuweka chini silaha.

Msemaji wa serikali ya Israel anasema, makundi ya Wapalestina yamependekeza pekee kusitisha makombora yanayofyetuliwa toka Gaza dhidi ya maeneo ya Israel, badala yake Israel ilitakiwa isitishe hujuma zake dhidi ya Gaza na maeneo ya Ukingo wa magharibi.

Msemaji wa serikali ya Israel anasema pendekezo hilo halina maana yoyote.

Pendekezo hilo la kuweka chini silaha lilitolewa na vyama vya FATAH na Djihad.

Wakati huo huo jeshi la Israel limempiga risasi na kumuuwa mwanaharakati mmoja wa Hamas kaskazini mwa Gaza.

Nacho Chama cha Hamas kimemshtumu Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas kwa kulazimisha kile wanachokiita masharti mapya yasiyokubalika juu ya kuunda serikali ya muungano.

Abbas anajaribu kuifungamanisha serikali mpya na kuachiliwa huru kwa mwanajeshi wa Israel aliyetekwa nyara na wapiganaji wa Kipalestina mwezi June, na pia kuzuia mashambulizi ya Hamas na makundi mengine dhidi ya Israel.