1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Kansela Merkel wa Ujerumani afanya ziara mashariki ya kati

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDa

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewasili nchini Israel kuendelea na ziara ya mashariki ya kati yenye lengo la kufufua juhudi za kuleta amani baina ya waisralei na wapalestina.

Bibi Merkel ambae ni mwenyekiti wa sasa wa baraza la Umoja wa Ulaya amefanya mazungumzo na waziri Mkuu wa Israel bwana Ehud Olmert mjini Jerusalem.

Leo anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas katika mji wa Ramallah.

Katika ziara yake ,kiongozi huyo wa Ujerumani ameshaitembelea Jordan ambapo alikutana na mfalme Abdullah.Bibi Merkel pia ataenda Lebanon ambako atamaliza ziara yake ya siku tatu katika mashariki ya kati.