1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem.Marekani kuongeza msaada wa kijeshi kwa Israel.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdt

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amethibitisha kuwa Marekani inapanga ongezeko kubwa la msaada wa kijeshi kwa nchi yake. Olmert amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wake wa kila wiki wa baraza la mawaziri kuwa Marekani imekubali ongezeko la asilimia 25 kwa zaidi ya dola bilioni 30 katika muda wa miaka 10 ijayo.

Tangazo hilo linafuatia ripoti kuwa Marekani inatayarisha makubaliano kadha ya silaha yanayolenga kuongeza uwezo wa kijeshi wa Saudi Arabia na mataifa kadha washirika wa Marekani katika mashariki ya kati.

Hatua hiyo , ambayo inasemekana kujumuisha mauzo ya silaha za kisasa zitakazokuwa na thamani ya dola bilioni 20 , inaonekana kuwa juhudi za kusaidia kupambana na ushawishi wa Iran unaoongezeka katika eneo hilo.