1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.Mkutano wa pande tatu wamalizika bila ya makubaliano yoyote

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQg

Mkutano wa pande tatu kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice, waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas umemalizika mjini Jerusalem bila ya kufikiwa makubaliano yoyote.

Baada ya mkutano huo waziri wa mambo ya nje Condoleeza Rice aliwaambia waandishi wa habari kwamba mabwana Olmert na Abbas watakutana tena hivi karibuni.

Mkutano huo ulikabiliwa na kutoelewana kuhusu serikali mpya ya umoja ya eneo la Palestina kati ya vyama vya Hamas na Fatah.

Kabla ya mazungumzo hayo Israel na Marekani zilisema kuwa hazitaitambua serikali hiyo ya umoja mpaka masharti yaliyowekwa yatimizwe.

Masharti hayo ni pamoja na kuitambua Israel na kulaani vitendo vya vurugu.