1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.Mwanamke mmoja auwawa katika shambulio la roketi

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsY

Vyombo vya habari nchini Israel vimeripoti juu ya kuuwawa kwa mwanamke mmoja na mumewe kujeruhiwa katika shambulio la roketi iliyolenga nyumba yao katika mji wa Sderot.

Mji wa Sderot uko umbali wa kilomita tano kaskazini mwa mpaka wa Gaza.

Makundi ya Jihad na hamas yamedai kuhusika na shambnulio hilo.

Shambulio hilo limetokea wiki moja baada ya wapalestina 19 kuuwawa katika shambulio lililo tekelezwa na Israel katika mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa Palestina.

Wengi wa waliouwawa ni wanawake na watoto.