1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert adinda kujiuzulu

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5f

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amewaambia waisrael hatojiuzulu kufuatia ripoti iliyoikosoa vikali serikali yake kutokana na kujiingiza vitani mwaka jana dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon.

Akitoa hotuba yake kupitia televisheni kiongozi huyo wa Israel amekiri kwamba makosa yalitendeka kwenye vita hivyo.

Tume ya serikali iliyoteuliwa na bwana Olmert mwenyewe imekosoa jinsi mambo yalivyoendeshwa na serikali katika mapambano hayo.Tume hiyo imekosoa uamuzi wa waziri mkuu pamoja na waziri wa ulinzi Amir Peretz na mkuu wa zamani wa jeshi Dan Halutz aliyejiuzulu mwezi Januari.

Olmert na Peretz wanaendelea kupata shinikizo la kuwataka wajiuzulu.