1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert azidi kukabiliwa na shinikizo za kutaka ajiuzulu

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5N

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert anapanga kukutana na mawaziri wake hii leo kutangaza jopo litakaloangalia utekelezaji wa ripoti iliyotolewa na tume iliyokuwa ikichunguza vita vya Israel dhidi ya Hezbollah.

Waziri mkuu Olmert anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzlu baada ya ripoti hiyo ya tume ya Winograd kumkosoa kwa jinsi alivyoendesha vita hivyo nchini Lebanon.

Shinikizo za kumtaka ajiuzulu zimepata nguvu zaidi tangu hapo jana baada ya waziri wake mmoja kujiuzulu akisema umma wa Israel umepoteza imani na bwana Olmert.Pigo kubwa kwa bwana Olmert limetoka kwa waziri wake wa mambo ya nje Tzipi Livni ambaye amenukuliwa na kituo kimoja cha Televisheni akisema waziri mkuu Olmert lazima ajiuzulu.