1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Wapalestina na waisrael wakubaliana kukutana kila babada ya wiki mbili

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEw

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleza Rice ametangaza kuwa viongozi wa Israel na Palestina wamekubaliana kuwa na mazungumzo kila baada ya wiki mbili kwa nia ya kujenga uaminifu miongoni mwao kuelekea kwenye amani ya mashariki ya kati.

Hata hivyo Waziri wa Nje wa Israel Tzipi Livni amesema kuwa kwa sasa kufikiwa kwa mkataba wa amani haiwezekani, lakini Israel imekubali kuwa na mazungumzo hayo juu ya hali ya kuanzishwa kwa taifa la Palestina, na mahitaji ya usalama wa Israel.

Condeleza Rice ametangaza hayo baada ya kufanya mazungumzo kadhaa na viongozi wa Israel na Palestina, katika juhudi za Marekani kufufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.

Taarifa hiyo Condoleza Rice inakuja mnamo wakati ambapo viongozi wa nchi za Kiarabu wanajianda kuanza mkutano wao wa kilele hii leo huko Riyadhi Saudi Arabia.

Mkutano huo unatarajiwa kufufua rasmi juhudi zilizokuwa zikifanywa na umoja huo katika kutafuta amani ya mashariki ya kati na kujihusisha kikamilifu katika mazungumzo na taifa la kiyahudi