1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Chad lakabiliwa na mapigano makali kabisa

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ59

NDJAMENA

Vikosi vya Chad vikiimarishwa na silaha nyingi za kisasa vinaweka upinzani mkali dhidi ya mashambulizi ya waasi ya takriban miaka 20 lakini waasi katika taifa hilo la Afrika ya Kati inaonekana kuwa wako tayari kwa mapigano hadi mwisho.

Maafisa wa serikali,waasi,waangalizi wa kigeni na wataalamu wote wanakubali kwamba mapigano yaliozuka mashariki mwa nchi hiyo tokea tarehe 26 mwezi wa Novemba ni mabaya kabisa tokea Rais Idriss Deby anyakuwe madaraka hapo mwezi wa Desemba mwaka 1990.

Hata hivyo jeshi linaweza kuhimili mashambulizi kwa kiasi kikubwa kutokana na silaha mpya zinazogharimiwa na utajiri wa mafuta wa hivi karibuni kabisa wa nchi hiyo.

Makundi mawili makuu ya waasi ya RFC na UFDD yamesema hivi karibuni yanaratibu mapambano yao dhidi ya utawala wa Deby.