1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la MONUC latuma wafanyakazi wake wa kiraia kusaidia kulinda amani

Kanyunyu John5 Februari 2009

MONUC yalaumiwa kutowalinda raia dhidi ya waasi wa LRA

https://p.dw.com/p/GnZs

Katika juhudi za kulinda raia dhidi ya mashambulio yanayofanywa kwenye operesheni ya pamoja, inayoendelea kufanywa na Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda dhidi ya waasi wa FDLR, jeshi la Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUC, limetuma wafanyakazi wake wa kiraia katika baadhi ya maeneo, kusaidiana na vikosi vya jeshi hilo kulinda raia.

Wakati huo huo shirika la madaktari wasio na mipaka limelaumu jeshi hilo la MONUC, kutolinda raia katika wilaya ya Dunga dhidi ya mashambulio yanayofanywa na waasi wa Uganda wa LRA.

Sikiliza ripioti ya mwandishi wetu wa Goma John Kanyunyu