1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Nigeria laendesha oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram

Admin.WagnerD20 Mei 2013

Mapigano makali yanaedelea nchini Nigeria kati ya Jeshi la Nigeria na wapaiganaji wa kundi la Boko Haram,ikiwa ni siku ya tano toka Jeshi la Nigeria kufanya operesheni ya kupambana na Boko haram mji wa Maiduguri

https://p.dw.com/p/18axE
Wanajeshi wa Nigeria.wakipambana na wapiganaji wa Boko Haram
Wanajeshi wa Nigeria.wakipambana na wapiganaji wa Boko HaramPicha: picture-alliance/dpa

Mji muhimu wa kaskazini mashariki mwa Nigeri,Maiduguri ulifungwa na kufanya usafiri kuwa mgumu baada ya jeshi la Nigeria kuendesha opareshini ya masaa 24 ya kupambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi la Nigeria General Brigadier Chris Olukolade amesema kuwa katika operesheni hiyo jumla ya waasi 17 wa Boko Haram wameuawa na wanajeshi watatu wa jeshi la Nigeria pia wameuawa. Kufuatia maelezo yaliotolewa na jeshi la Nigeria katika miji mitatu,Jeshi hilo limesema kampeni hiyo inalenga kupambana na kundi la Boko Harm ambalo linataka kusimamisha utawala wa kiisalamu Kaskazini mwa Nigeria.Jeshi la Nigeria limengaza kuwasemehe wapiganaji wa Boko haram watakaojisalimisha.

Katika mji wa Adamawa,wanajeshi 150 walimwaga na wengine 100 ambao hawakutarajiwa na kuharibu kambi kaddhaa karibu na mji wa Borno.Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari juma lililopita katika miji ya Borno Yobe na Adamawa. Katika maelezo yake Rais Goodluck Jonathan amewataka wapiaganaji wa kundi la Boko Haram kuweka silaha chini na kuchukua hatua ya kujisalimisha,wakati ambapo akiandaa kamati ya kuangalia uwezekano wa kujisalimisha wapiganaji hao .

Boko Haram bado inashikilia msimamo wake.

Kwa upande wake kiongozi wa kundi la Bokoharam Abubakar Shekau amekataa wito wa Rais Goodluck Jonathan wa kujisalimisha wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar ShekauPicha: AP

Msamaha kama huo kwa wapiganaji wa kundi la Boko haram ulisaidia kumaliza mapiagano katika eneo la Niger Delta mwaka 2009 baada ya mapigano ambayo yalisimamaisha shughuli ya uchimbaji mafuta kwa kadhaa.

Wachambuzi wana hofu kuwa huenda hatua ya jeshi la Nigeria kufanya opareshini hiyo dhidi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram,ikakwamisha suluhisho la kisiasa la kumaliza mapigano kati ya serikali na kundi la Boko Haram.

Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ukiukaji wa haki za binadam katika opareshini hiyo.Mawasiliano ya simu yamekatwa katika miji ya mashariki ya Kaskazini mwa Nigeria kuzuwia wapiganji wa Boko Haram kuwasliana.

Mapigano kati ya serikali na Boko Haram yamegharimu maisha ya zaidi ya watu 3,600 yakiwemo mauaji yaliofanywa na vyombo vya usalama tangu mwaka 2009

Mwandishi: Hashimu Gulana/ AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman