1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi lashambulia waasi wa PKK.

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVev

Istanbul. Jeshi la Uturuki limesema kuwa limefanya mashambulizi dhidi ya waasi wa Kikurd kaskazini mwa Iraq, na kusababisha hasara kubwa kwa kundi la wapiganaji waliokuwa zaidi ya 50. Jeshi hilo limesema lilitumia silaha za kawaida pamoja na ndege za kivita katika operesheni hiyo , na kwamba hakuna majeshi ya ardhini yaliyotumika kuingia katika ardhi ya Iraq. Siku ya Ijumaa waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na baraza lake la mawaziri waliidhinisha jeshi kufanya operesheni hiyo kuvuka mpaka dhidi ya wapiganaji wa chama cha wafanyakazi wa Kikurd cha PKK. Uturuki imeweka wanajeshi wapatao 100,000 karibu na eneo la mpaka milimani , likisaidiwa na vifaru , mizinga na ndege za kijeshi.