1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi Tunisia lawafunga wabunge wawili

Grace Kabogo
22 Septemba 2021

Jaji wa kijeshi nchini Tunisia amewahukumu kwenda jela wabunge wawili wa chama chenye itikadi kali za Kiislamu cha Karama.

https://p.dw.com/p/40ede
Tunesien | Militär | Beisetzung Mohamed Taher Ayari
Picha: dpa/picture alliance

Hukumu hiyo imetolewa wakati ambapo wasiwasi kuhusu suala la haki za biandamu unaongezeka, baada ya rais kuchukua mamlaka yote mwezi Julai.

Mahakama hiyo imewafungwa Nidal Saudi na Saif Eddine Makhlouf, kiongozi wa chama cha Karama na mkosoaji wa mara kwa mara wa Rais Kais Saied bungeni.

Hukumu hiyo inaifanya idadi ya wabunge waliofungwa kufikia watano.

Taarifa iliyotolewa na mahakama ya kijeshi imesema jaji huyo aliamuru Makhlouf afungwe kwa sababu alitoa kitisho kwa jaji wa kijeshi na kuwahutumu majaji wa kijeshi kwa kuhusika katika kile Makhlouf alichokieleza kama mapinduzi.

Rais Saied alimfuta kazi waziri mkuu, alilisimamisha bunge na kuchukua madaraka kamili Julai 25, hali inayozusha wasiwasi kuhusu nia yake.

Makundi ya haki za binaadamu yameshinikiza kuachiwa kwa mbunge mwingine, Yassin Ayari na yamekosoa matumizi ya mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za raia.