1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jinsi Elombo Bolayela alivyofanikiwa kuwa mbunge nchini Ujerumani

6 Desemba 2012

Kwamba wajerumani wenye asili ya kituruki wanajishughulisha na pirika pirika za kisiasa humu nchini si jambo jipya-jipya lakini ni kusikia kwamba mtu mwenye asili ya kiafrika akiwa mbunge

https://p.dw.com/p/16wqL
Wawakilishi katika bunge la jimbo la BremenPicha: DW

Wabunge wenye asili ya kigeni si jambo jipya nchini Ujerumani.Cem Özdemir ambae ni mwenyekiti wa chama cha walinzi wa mazingira au Lale Akgün aliyewahi kuwa mbunge wa chama cha Social Democratic hakuna asiyewajua humu nchini.Lakini mbunge mwenye asili ya kiafrika"!Hajawahi kushuhudiwa hadi sasa . Tangu mwaka mmoja uliopita hali hiyo imebadilika!Kuna mbunge mwenye asili ya kiafrika katika bunge moja la jimbo la kaskazini mwa Ujerumani.Jina lake ni Elombo Bolayela-anakiwakilisha chama cha Social Democratic katika bunge la jimbo la Bremen.Elombo Bolayela aliipa kisogo Kongo alipokuwa na umri wa miaka 27,alitapia maisha kama mkimbizi nchini Ujerumani na sasa amekuja kuwa kile wanasiasa wanachopendelea sana kukiita "amefanikiwa kujiambatanisha na hali ya maisha ya humu nchini"Katika bunge la jimbo la Bremen,Elombo Bolayela anajishughulisha pia kwa hivyo na masuala yanayowahusu wahamiaji.

Elombo Bolayela anafanyakazi katika duka la zana za nyumbani na ujenzi tangu miaka 13 iliyopita.Kila mtu anamjua na kila mtu anamsifu.Huko ndiko mzaliwa huyo wa Kongo alikojijengea maisha mepya.Anakalia kiti katika kamati ya uongozi ya baraza la wawakilishi wa wafanyakazi.Kwasababu Bolayela anependa kujishughulisha na kuwajibika.Tangu mwaka mmoja uliopita amejipatia jukwaa jipya:Amekuwa mbunge katika bunge la jimbo la Bremen-akiwa mtu wa kwanza na pekee mwenye asili ya kiafrika kakalia kiti katika bunge nchini Ujerumani.Hajawahi Bolayela hata siku moja kuotea kama itafika siku atajishughulisha na siasa nchini Ujerumani.Wenzake katika chama cha Social Democratic-SPD,ingawa walimuweka nafasi ya nyuma katika orodha ya uchaguzi,lakini wapiga kura wa Bremen walikuwa wakimtaka na kutokana na kura nyingi za moja kwa moja,akamaliza wa sita kati ya waliojikingia kura nyingi katika orodha ya chama cha SPD anasema Elombo Bolayela"Nimezoweyana sana na watu huku,Watu wananipenda.Pengine hali hiyo inatokana na mtazamo wangu kwamba binaadam ni wema.Hilo kwangu ni bayana.Nna ya maana ya kuzungumzia."

Deutschland Bremen Bürgerschaft Abgeordneter Elombo Bolayela
Elombo Bolayela bungeni mjini BremenPicha: DW

Mwanzoni maisha yake hayakuwa rahisi nchini Ujerumani.Nchi alikozaliwa,Zaire,inayojulikana hivi sasa kama jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,alilazimika kuipa kisogo miaka 20 iliyopita.Wakati ule mtawala wa kiimla,Mobutu Seseseko ndie aliyekuweko madarakani.Hakufanya la maana kwa nchi yake.Shughuli za kiuchumi zilivurugika na hali ya maisha ya wananchi kuporomoka.Elombo Bolayela anakumbukla jinsi vugu vugu la wapenda demokrasia lilivyochipuka katika miaka ya 90.

"Nilipokuwa mwanafunzi mnamo mwaka 1991 nilisikia kwa mara ya kwanza kabisa neno "Demokrasia" na nikamuuliza professor"Neno hilo manaake nini?Akasema "Huo ni mfumo bora kabisa wa kisiasa nchi inaoweza kuwa nao na mfumo huo ndio unaorahisisha maendeleo.Kila mmoja wetu anakuwa na nafasi ya kuwa waziri au mwalimu na kadhalika.Na barabara nyingi zitakuwepo,ni dhahir."Anasema Bolayela.

Mwamko huo ulimzinduwa pia kijana huyo.February 16 mwaka 1992,ilikuwa siku ya jumapili,alijiunga na maelfu ya wenzake na kuteremka majiani kuandamana dhidi ya Mobutu.Kilichopangwa yalikuwa maendeleo makubwa ya amani.Watu walikuwa wakiimba majiani-mji mzima ukinguruma-anakumbuka Bolayela.Lakini maandamano hayo yalimalizika kwa damu kumwagika pale wanajeshi walipowafyetulia risasi waandamanaji.Watu wasiopungua 200 waliuliwa.Hata Bolayela alipigwa risasi.Siku ya pili yake akakimbia- msitu na nyika mpaka akafika Ujerumani.Kwa miaka alikuwa akipigania haki ya kuishi kama mkimbizi nchini Ujerumani.Kilichokuwa kikimpa moyo aendelee na juhudi zake nchini Ujerumani,anasema Bolayela kwanza ni watu waliokuwa wakimuunga mkono,na baadae juhudi zake katika kulitumia kanisa na kujiunga na kwaya ya kanisa.

Elombo Bolayela ndie aliyesaiadia kuanzisha kwaya hiyo na pia kujishughulisha na harakati za kisiasa.Wenzake katika bunge la jimbo la Bremen wanamsifu na kumthamini.Amechangia kuandaa mswaada wa sheria unaozungumzia nafasi bora kwa wanafunzi wa kigeni.Ni ufanisi mkubwa huo ikizingatiwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tu tangu aanze kukalia kiti katika bunge la jimbo la Bremen anasifu mwenyekiti wa kundi la wabunge wa SPD Björn Tschöpe.

Mobutu ameshapinduliwa na nchi hiyo kwa mujibu wa katiba ni ya kidemkrasi.Yanayotokea huko lakini Bolayela anayafuatilizia kutoka huku huku Ujerumani,anaona jinsi wananchi wanavyotaabika na jinsi maafisa wa serikali wanmavyotumia vibaya madaraka yao.

Hana dhamiri ya kuingilia kati huko,anasema,kinyume na huku anakoishi ambako anawajibika awezavyo wanamsifu wabunge wenzake na kumshukuria.

CDU Parteitag 05.12.2012
Wajumbe katika mkutano mkuu wa chama cha CDU mjini HannoverPicha: Reuters

Kuwa na wabunge wenye asili ya kigeni ni ngao inayotumiwa na vyama vya kisiasa katika juhudi zao za kuania kura za jamii hizo za wahamiaji uchaguzi unapoitishwa.Cem Özdemir wa Chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne na Lale Akgün wa Social Democratic SPD walikuwa wanasiasa wa kwanza wenye asili ya kigeni waliofanikiwa kujijenga kataika uwanja wa kisiasa nje ya nchi yao ya asili.Hata chama cha kihafidhina cha CDU kinaonyesha kuufuata mkondo huo.Katika mkutano wao mkuu hivi karibuni mjini Hannover,wajumbe wamewachagua wanasiasa watatu-wote wanawake na wote wana asili ya Uturuki kukalia viti vya kamati ya uongozi ya chama hicho.Wanne kuingia katika taasisi hiyo inayopitisha maamuzi ya CDU kwa daraja ya taifa ni kijana mwenye umri wa miaka 24 mwenye asili ya Moroko.Mkondo huu ni mpya hasa inapozingatiwa kwamba kawaida wapiga kura wenye asili ya kigeni huelemea zaidi upande wa vyama vya kijamaa na mrengo wa shoto badala ya chma cha kihafidhiana .

Uchunguzi wa maoni waliyofanyiwa wajerumani wenye asili ya kituruki katika mwaka 2009 na taasisi ya "Data for 4" umebainisha asili mia 10 tu ya walioulizwa maoni yao wametamka wanakipigia kura chama cha CDU uchaguzi unapoitishwa.Badala yake asili mia 55 wamesema wanakipigia kura chama cha SPD na asili mia 23 chama cha walinzi wa mazingira.

Mwandishi/Sandner Philipp/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Yusuf Saumu