1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jinsi ya kuwanusuru watoto wasiteswe majumbani

Oummilkheir27 Desemba 2007

Ni miongoni mwa yaliyochambuliwa na wahariri wa Ujerumani

https://p.dw.com/p/Cgja
Mshahara usiwe chini ya Yuro sabaa na senti hamsini kwa saaPicha: AP

Mjadala unaoendelea kuhusu kiwango cha chini cha mishahara,kufukuzwa wanadiplomasia wawili kutoka Afghanistan na kuwalinda watoto dhidi ya mateso ndizo mada zilizopewa umuhimu mkubwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanze basi na juhudi za kuepusha watoto wasiteswe.Kutokana na visa vya hivi karibuni,gazeti la mjini Postdam- MÄRKISCHE ALLGEMEINE linaandika:

„Japo kama ripoti kutoka München na Beratzhausen zinahuzunisha na ku,hata hivyo ripoti hizotisha, hazimaanishi lakini kwamba hali jumla ndivyo ilivyo hivyo.Ni sawa kabisa kwamba serikali lazma iingilie kati,ifanye kila la kufanya ili watoto wanaotokana na familia zenye shida watambulikane haraka na kusaidiwa.Hata hivyo haitakua sawa kuwafanya watu waamini kwamba wanasiasa wanaweza kuzuwia moja kwa moja watoto wasiuliwe au wasiteswe.Mipaka ya serikali inaishia pale familia inapoanzia.“

Gazeti la NORDBAYERISCHE KURIER la mjini Bayreuth linaandika:

„Wajerumani wanalalamika jamii haishughulishwi na kitu na haipendi watoto,lakini wakati huo huo hata watoto wa jirani hawasubutu kuwarudi.Serikali inashindwa,hasa inapojaribu kujigeuza chombo cha kurekebisha kila kitu.Maafa yanayowakumba binaadam hayawezi yote kuzuwilika,lakini yanapotokea kila kwa mara,yanaashiria mzozo ambao unaweza kuepukwa ikiwa watu watafunguliana nyoyo na kusaidiana..“

Hayo ni maoni ya gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER la mjini Bayreuth kuhusu jinsi ya kuwanusuru watoto .Mada ya pili magazetini ni kuhusu mjadala unaoendelea wa kiwango cha chini cha mishahara.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:

Kwa mtazamo wa kijuu juu,mtu anaweza kusema mfumo uliochaguliwa na Ujerumani unatatanisha.Kwanza serikali inashindwa kuafikiana juu ya kiwango cha chini cha mishahara.Pili inaachia baadhi ya makundi ya wafanyakazi,mfano watumishi wa posta wanaopeleka barua majumbani walipwe vyengine kabisa na kuruhusu posta iendelee kuidhibiti hali ya mambo.Na wakati huo huo kila mtu anashangiria.Pengine mwaka 2008 utaleta kiwango cha kweli cha mishahara ya chini kwa wafanyakazi wote.Si kizungumkuti hicho au vipi?Linajiuliza gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.

Mada ya mwisho magazetini inahusu uamuzi wa serikali ya Afghanistan wa kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Ulaya kwa makosa ya kuzungumza ,bila ya ruhusa, na wanamgambo wa Taliban.Gazeti la TAGESPIFGEL linaandika:

Pengine wanadiplomasia hao wamekiuka mstari mwekundu.Hata hivyo,ukweli unasalia pale pale: pekee njia za kijeshi , bila ya mazungumzo pamoja na wapinzani wa serikali kuu,amani haiwezi kupatikana nchini Afghanistan.