1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jitihada ya tiba ya upasuaji EAC

22 Julai 2015

Nchi za Afrika mashariki zimeanzisha mkakati wa pamoja wa kuzalisha wataalamu wa upasuaji kwa ajili ya kukabiliana na pengo kubwa lililopo ambalo linasabisha huduma hiyo kutopatikana kirahisi katika baadhi ya maeneo.

https://p.dw.com/p/1G3Ja
Tansania, Fahrzeug für medizinische Hilfe
Gari maalumu au kontena la kutoa tiba za upasuaji katika maeneo ya jijini Dar es SalaamPicha: DW/G. Njogopa

Nchi hizo ziko mbioni kunufaika na mpango mpya baada ya kuzinduliwa kwa mfumo wa kisasa unaotumia gari ama kontena maalumu kufundishia wataalamu wa upasuaji. Tayari kontena hilo limeanza kufanya kazi nchini Tanzania likiwafunza madaktari wa upasuaji katika vyuo vya tiba vilivyoko jijini Dar es Salaam na baadaye litasafirishwa katika miji mingine ikiwamo Mwanza na Arusha. Kwa kufahamu zaidi sikiliza makala iliyoandaliwa na George Njogopa. Kusikiliza makala bonyeza kitufe cha kusikilizia masikioni hapo chini.