1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jitihada za kujumuisha tamaduni tofauti hazikufanikiwa Ujerumani

Kabogo Grace Patricia17 Oktoba 2010

Matamshi hayo yametolewa na Kansela Angela Merkel katika hotuba yake kwa chama cha vijana wa chama chake cha CDU.

https://p.dw.com/p/Pg0b
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: dapd

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema kuwa jitahada za kujenga jamii ya tamaduni tofauti nchini humo zimeshindwa vibaya. Merkel alitamka hayo alipokuwa akihutubia chama cha vijana wa chama chake cha kihafidhina CDU.

Kansela Merkel ametamka hayo baada ya mwanasiasa mwenzake wa kihafidhina Horst Seehofer, siku ya Ijumaa kusema kuwa Ujerumani sio nchi ya wahamiaji na kwamba kukosekana kwa wafanyakazi wenye ujuzi kusionekane kama kuwepo uhuru wa kile alichokiita "uhamiaji usiodhibitiwa."

Wakati huo huo, mwanasiasa wa chama cha Kijani, Jürgen Trittin ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag kuwa Seehofer anachochea misimamo mikali kwa matamshi yake hayo. Trittin ameliambia gazeti hilo kuwa wafanyakazi wenye ujuzi wapaswa kutiwa moyo kuja Ujerumani na irahisishwe kwa watu hao kuja Ujerumani na kufanya kazi.