1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joe Biden kukutana na Yoshihide Suga

Amina Mjahid
16 Aprili 2021

Rais wa Marekani, Joe Biden, atamkaribisha Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga, katika ikulu ya White House mjini Washington, katika mkutano unaotajwa kuwa na ujumbe mzito kwa China

https://p.dw.com/p/3s8ff
USA | Washington | Rede Präsident Joe Biden
Picha: Andrew Harnik/AFP/Getty Images

Mkutano huo kati ya Rais Biden na Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga unatajwa kuwa unatuma ujumbe mzito kwa China, ambayo imekuwa ikidai kwamba Marekani na washirika wake wanazidi kupoteza ushawishi katika anga za kimataifa.

Maoni kama hayo kuelekea Marekani yalianza kutolewa na China baada ya Rais aliyepita Donald Trump, kuamua kupunguza ushiriki wa Marekani katika matukio na mikataba mbali mbali ya kimataifa.

Akizungumzia kuhusu mkutano wa viongozi hao wawili na ujumbe wanaoutuma kuelekea China, waziri wa habari wa Marekani, Jen Psaki, alisema na hapa namnukuu „mkakati wetu kuelekea China pamoja na jinsi tunavyotaka kuratibu mashirikiano yetu katika hilo, itakua ni moja kati ya vitu vitakavyojadiiwa katika mkutano huo" mwisho wa kumnukuu.

Kabla ya kwenda Washington Waziri Mkuu Suga lieleza jinsi alivyokuwa na hamu ya kuonana na Biden licha ya kuendelea kuwepo kwa janga la corona. Suga alidai tukio hilo linatoa ujumbe kwa Marekani kwamba Japan ni mshirika wake muhimu hususani katika kushughulia masuala ya usalama.

Japan US Premierminister Yoshihide Suga
Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide SugaPicha: Sadayuki Goto/AP/picture alliance

Nchi hizo mbili zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika kukuza teknolojia zao ili kupunguza kuitegemea China katika ugavi wa baadhi ya teknolojia. Katika kikao hicho Japan inategema kutangaza uwekezaji wa teknolojia ya 5G ambayo itakuwa kama mbadala wa teknolojia hiyo kutoka China.

Ukiachilia hayo nchi hizo mbili zinategema kutangaza ahadi zao za kupunguza gesi chafu katika upande wa sera za mabadiliko ya tabianchi. Hayo yanafanyika kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa wiki ijayo kati ya Biden na viongozi wengine 40 wa dunia.

Serikali ya Biden pia inaweza kuwa na maombi zito kuelekea Japan kwa kumtaka Waziri Mkuu Suga kutoa tangazo kwa umma la kuunga mkono Taiwan. China ambayo inaona Taiwan kama ni kati ya sehemu yake inayojitawala yenyewe, ilituma ndege zake za kivita na mabomu karibu na Taiwan hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alishamuonya mwezake wa Japan kabla ya safari ya Waziri Mkuu Suga kwenda Marekani na kuisihi Japan isiingilie katika mvutano wake na Marekani.

Chanzo: APE