1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joe Biden, mgombea mwenza wa Barack Obama

Nijimbere, Gregoire24 Agosti 2008

Barack Obama amesubiri siku mbili kabla ya kufunguliwa kikao cha mkutano mkuu wa chama chake cha demokrate ambapo atateuliwa rasmi muakilishi wa chama kwenye uchaguzi wa urais na kutangaza mgombea mwenza, Joe Biden.

https://p.dw.com/p/F3tZ
Barack Obama na Joe BidenPicha: AP

Barack Obama anayetazamiwa kukiwakilisha chama cha demokrate kwenye uchaguzi wa urais nchini Marekani, ameonekana hadharani akiwa pamoja na mgombea mwenza wake, seneta Joe Biden. Maelfu ya wafuasi wa chama cha demokrate wamemiminika katika mji wa Springfield jimbo la Illinois kuwashangilia wawakilishi wao. Barack Obama alimsifu seneta Biden na kusema kuwa wote pamoja wataipa Marekani kwenye muelekeo mzuri. Joe Biden amesisitiza juu ya matatizo ya kiuchumi na sera na nje za Marekani na kusema kuwa nchi inahitaji kuchukuwa muelekeo mpya.

Joe Biden amesema huu sio wakati wa kawaida:

''Mabibi na mabwana huu sio wakati wa kawaida, huu sio uchaguzi wa kawaida na hii huenda ni bahati ya mwisho ya kuigeuza Marekani tuipendayo na kurejesha imani yake''.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema chaguo la Joe Biden, seneta wa muda mrefu na mzoefu wa masuala ya nchi za kigeni, limeonekana kama kuziba kasoro ya Barack Obama katika masuala ya kimataifa.


Barack Obama amechagua jimbo lake la Illinois kumtangaza mgombea mwenza, pale pale alipotangazia kwamba atagombea kiti cha urais wa Marekani miezi 6 iliyopita.