1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za amani ya mashariki ya kati zajadiliwa mjini New York

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNJ

New York:

Wawakilishi wa pande nne zinazosimamia utaratibu wa amani ya mashariki ya kati,wanatazamiwa kukutana hii leo,kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New-York kuzungumzia maandalizi ya mkutano wa amani kati ya Israel na Palastina,unaotazamiwa kuitishwa mwezi November mwaka huu.Katika mkutano huo wa leo, wawakilishi wa pande nne,ambazo ni Umoja wa mataifa,Marekani,Urusi na Umoja wa ulaya watasikiliza ripoti ya kwanza ya waziri mkuu wa zamani wa Uengereza Tony Blair,kuhusu hali ya mashariki ya kati.Itakumbukwa kwamba Tony Blair aliteuliwa mwezi June uliopita kuwa muakilishi wa pande nne zinazosimamia juhudi za amani ya mashariki ya kati.Marekani,Umoja wa mataifa,Umoja wa Ulaya na Urusi,mwaka 2003 waliandaa mpango wa amani uliolengwa kuundwa taifa la Palastina ifikapo mwaka 2005-lakini mpango huo umekwama.