1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuleta utulivu zinaendelezwa nchini Irak

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCir

Mkutano wa suluhu ya taifa unatazamiwa kuitishwa hii leo mjini Baghdad nchini Irak.Walioalikwa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi wa makundi tofauti ya kisiasa na kidini,waakiwemo pia wawakilishi wa chama cha Baath cha rais aliyepinduliwa Saddam Hussein.Sauti zinapazwa kudai mkutano huo ususiwe.Waziri mkuu Nuri al-Maliki amemhakikishia kwa simu rais George w. Bush wa Marekani,atautumia mkutano huo ili kuleta hali ya utulivu nchini humo.Hali ya vurugu na ukosefu wa sheria inazidi kupata nguvu nchini Irak.Serikali ya Irak imepinga kuitishwa mkutano wa kimataifa kuzungumzia amani ya nchi hiyo kwa hoja mkutano kama huo utakiuka mamlaka yake kama taifa.