1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

110509 Israel USA

Charo Josephat/Peter Philip11 Mei 2009

Waziri mkuu wa Israel ataka kuanza tena mazungumzo

https://p.dw.com/p/Ho2U
Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Urusi inataka mazungumzo ya maana kuhusu mchakato wa kutafuta amani ya Mashariki kupitia kikao cha mawaziri cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kinachoanza leo mjini New York nchini Marekani. Rais wa Marekani Barack Obama pia ameashiria kuchukua hatua za kuzipiga jeki juhudi za kutafuta amani ya Mashariki. Lakin je hali iko vipi kati ya utawala mpya wa Israel na wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina?

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema leo kwamba anataka kuanzisha tena mazungumzo ya amani na Wapalestina. Kiongozi huyo ameyasema hayo katika mji wa mapumziko wa Sharm el Sheikh nchini Misri wakati alipokutana na mwenyeji wake raia wa nchi hiyo, Hosni Mubarak. Hata hivyo kiongozi huyo hajathabitisha hadharani kuung amkono kuudhwa kwa dola huru la Palestina.

wasili hii leo katika mji wa mapumziko wa Sharm el Sheikh nchini Misri kwa mazungumzo yanayolenga kudhihirisha anaweza kuwa mshirika wa kutafuta amani kabla kuelekea mjini Washington Marekani.

Msemaji wa waziri wa mashauri ya kigeni wa Misri, Hossam Zaki, amesema Misri ilikuwa na matumaini kwamba waziri Netanyahu atathibitisha Israel imejitolea kwa dhati katika kufikiwa suluhu la kuundwa kwa taifa la Palestina.

Swala lengine litakalojitokeza kwenye mkutano wa leo ni juhudi za kumuokoa mwanajeshi wa Israel, Gilad Shalit, aliyekamatwa na Hamas mnamo mwaka 2006. Netanyahu pia alitarajiwa kumtaka rais wa Misri, Hosni Mubarak, amuunge mkono kukabiliana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Nchini Israel kumekuwa na mjadala kuhusu tofauti ya maoni kati ya nchi hiyo na Marekani. Rais wa Israel, Shimon Peres, alikuwa wa kwanza kuihakikishia Marekani kwamba urafiki kati ya nchi hizo mbili hautayumbishwa.

"Sioni nafasi ya uwezekano wa uhusiano wetu na Marekani kusambaratika."

Mahmud Abbas Rede in Ramallah Palästinenser
Rais Mahmoud AbbasPicha: AP

Kulikuwa na mpango wa kuweka vikwazo vipya kumshinikiza rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas, arejee kwenye meza ya mazungumzo na aitambue wazi Israel kama taifa la kiyahudi. Lakini rais Abbas anajinata kwa kuwa anajua matamshi hayo yatafuta kabisa uwezekno wa kumaliza ugomvi na kundi la Hamas.

"Taifa la kiyahudi ndo lipi. Tunaliita taifa la Israel. Mrtu anaweza kuliita atakavyo, lakini sikubali kuliita taifa la kiyahudi na nasema wazi. Nimeelza wazi kwamba sio kazi yangu kulipa jina taifa hili. Liiteni mnatakavyo, lakini mshipa haunipigi. Kwangu mimi kuna taifa moja tu la Israel ndani ya miapak ya mwaka wa 1967, lisilozidi wala kupungua kwa hata sentimeta moja. Sikubali jambo lolote lingine lile."

Marekani inataka kuzungumza na washirika wakuu na inasubiriwa ni matamshi gani yatakayotoka nchini humo katika majuma machache yajayo. Waziri mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu ana matumaini ya kuushangaza ulimwemgu.

"Nadhani kwa ushirikiano na rais Obama na rais Abbas tunaweza kufanya kinyume cha matarajio ya wakosoaji na kuushangaza ulimwengu."

Mkutano wa leo kati ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Misri, Hosni Mubarak, unafanyika kabla viongozi hao wawili kuzuru Marekani kwa mazungumzo tofauti na rais Barack Obamba kabla mwisho wa mwezi huu.