1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za Marekani mashariki ya kati

Admin.WagnerD9 Januari 2019

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema uamuzi wa Marekani wa kuondoa wanajeshi wake nchini Syria hautaathiri uwezo wa mataifa ya eneo hilo kulitokomeza kundi la IS pamoja na kuidhibiti Iran. 

https://p.dw.com/p/3BETF
Jordanien Ankunft Pompeo in Amman
Picha: picture-alliance/AP Photo A. Caballero-Reynolds

Mike Pompeo ametoa matamshi hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mjini Amman nchini Jordan kituo chake cha kwanza cha ziara yake ndefu ya kuzitembelea nchi nane za mashariki ya kati.

Pompeo amesisitiza kuwa serikali mjini Washington inatambua kuwa kitisho kikubwa katika kanda hiyo ni kundi la dola la kislaam (IS) na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na mataifa ya eneo hilo hata baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria.

Kadhalika mwanadiplomasia huyo wa Marekani amewahakikishia washirika wa nchi yake kuwa utawala wa rais Donald Trump katika wiki chache zijazo utaongeza maradufu shinikizo la kibiashara na kidiplomasia kwa Iran na kuwa kampeni dhidi ya nchi hiyo ya kiislam haitathiriwa na kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Syria.

Pompeo ambaye anakutana na maafisa wa Iraq leo akitokea Jordan, anaizuru mashariki ya kati wiki kadhaa baada ya rais Donald Trump kutangaza kuwa Marekani itaondoa vikosi vyake vyote vya askari 2000 nchini Syria uamuzi ambao na ulisababisha kujiuzulu kwa  waziri wa ulinzi James Mattis na kuzua wasiwasi mkubwa miongoni mwa washirka wake

Erdogan atofautiana na Bolton

Türkei Erdogan Rede
Picha: Getty Images/A. Altan

Ziara ya Pompeo ilianza hapo jana wakati mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton alikuwa akikamilisha ziara yake nchini Uturuki bila ya kukutana na rais Recep Tayyip Erdogan baada ya kutofautina kuhusu wapiganaji wa kikurdi nchini Syria.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa wawili hao walipangiwa kuwa na mkutano siku ya Jumanne kujadili hatma ya vikosi vya wakurdi vinavyopigana bega kwa bega na wanajeshi wa Marekani nchini Syria lakini mkutano huo haukufanyika.

Hapo jana rais wa Uturuki Reccip Tayyip Erdogan alimshambulia mshauri huyo wa usalama wa taifa  wa Marekani kwa matamshi yake ya kuitaka Uturuki itoe hakikisho la kutowadhuru wapiganaji wa kikurdi nchini Syria baada ya vikosi vya Marekani kuondoka.

Erdogan alisema John Bolton alifanya kosa kubwa kwa kuweka masharti ya jinsi jeshi la Uturuki linavyopaswa kuendesha shughuli zake baada ya Marekani kujiondoa nchini Syria.

IRak John Bolton, Sicherheitsberater von US-Präsident Trump
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Harnik

Uturuki inawazingatia wapiganaji wa kikurdi kuwa kundi la kigaidi na tawi la chama cha kikurdi  kilichopigwa marufuku cha PKK ambacho kimekuwa chanzo uasi na mapigano katika eneo la wakuri wengi la kusini mashariki ya Uturuki.

Uamuzi wa Washington kuwaunga mkono wapiganaji wa kuni hilo nchini Syria umeikasirisha serikali ya Uturuki.

Anthony Zinni ajiuzulu
Wakati huo huo mjumbe wa Marekani aliyekuwa na jukumu ya kusuluhisha mzozo baina ya Qatar na kundi la nchi  za kiarabu linaloongozwa na Saudi Arabia amejiuzulu.

Anthony Zinni amekiambia kituo kimoja cha televisheni kuwa ameamua kuondoka kwa sababu ya kukosena kwa nia thabiti ya viongozi wan chi hizo kumaliza mzozo huo kwa njia ya upatanishi uliopendekezwa na marekani.

Mwandishi: Rashid Chilumba/AFP/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu