1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za uokozi zakwama Pakistan

9 Agosti 2010

Mvua nying za masika zinaendelea kuzikwamisha harakati za uokozi katika maeneo mengi yaliyoathiriwa na mafuriko nchini Pakistan.

https://p.dw.com/p/OfBx
Maji yaliyotuama Kot Addu,Punjab- PakistanPicha: AP

Mafuriko hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa  katika kipindi cha miaka 80 ,yamesababisha vifo vya kiasi ya zaidi ya watu 1600 na wengine milioni 12 wameachwa bila makazi.

Ndege za uokozi zililazimika kuzikatiza safari za kuelekea kwenye maeneo yaliyoathiriwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa na kina kinachoongezeka cha maji ya mito iliyofurika iliyoyasomba madaraja.Hali hiyo imeshuhudiwa katika maeneo ya kaskazini magharibi ya Khyber-Pakhtunkwa ambako harakati za uokozi zimekwama hususan katika maeneo ya vijijini. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na janga hilo Jean–Maurice Ripert ameusisitizia umuhimu wa msaada wa jamii ya kimataifa

Pakistan Flut Katastrophe 2010 Flash-Galerie
Waathiriwa wa mafuriko wakiminyana kupata chakula cha msaada.Picha: AP

Mjumbe huyo aliizuru Pakistan ili kujionea hali halisi itakayomuwezesha kufanya tathmini kamili ya msaada unaohitajika.Kulingana na watabiri wa hali ya hewa,mito miengine 10 huenda ikafurika na mvua nyingi zaidi inatarajiwa kunyesha katika kipindi cha saa 48 zijazo katika eneo la kaskazini.Kwa upande wake Waziri Mkuu Yousef Raza Gilani amekiri kuwa nchi yake haina uwezo wa kukabiliana na janga hilo na ameitolea jamii ya kimataifa wito wa kuipa msaada wa dharura wa aina yoyote.Serikali ya Pakistan imenyoshewa kidole na wakazi wake walioathirika ambao bado hawajapata msaada wowote.