1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukwaa la Uchumi ulimwenguni:Cape Town

11 Juni 2009

Nchi nyingi za Afrika zapiga hodi Banki ya Afrika kuomba msaada.

https://p.dw.com/p/I7PA
Kofi AnnanPicha: picture-alliance/dpa

Serikali za kiafrika zimetakiwa katika Jukwaa la uchumi la Afrika mjini Capetown,Afrika Kusini kuutumia msukosuko wa hivi sasa wa uchumi ulimwenguni kusaidia kuhalalisha kutatua matatizo ya kimsingi yanayowafanya watiaji wengi raslimali kulikwepa bara la Afrika.

Kwa muujibu wa ripoti ya Banki Kuu ya Dunia nchi 17 kati ya 20 za Afrika ni taabau sana kufanya nazo biashara kutokana na vikwazo vingi vilivyowekwa.Ripoti ya Banki Kuu ya dunia,Banki Kuu ya Afrika na ya Jukwaa la Uchumi Ulimwenguni-World Economic Forum ilisema wiki hii kwamba mageuzi ya kiuchumi yaliochangia mno kuukuza haraka uchumi wa Afrika tangu kupita miongo kadhaa yamo sasa hatarini ya kuzorota kutokana na msukosuko wa sasa wa uchumi ulimwenguni.

Omari Issa,mkurugenzi-mtendaji wa Taasisi ya kuvutia raslimali barani Afrika yenye makao yake nchini Tanzania, amesema wakati sasa umewadia kuchukua hatua kurekebisha hali hiyo na sio tu kuzungumzia matatizo mfano ya miundombinu dhaifu na umangimeza uliofurutu ada.Huko Cape Town, Omari Issa alisema na ninamnukulu,

"Huu pengine ndio wakati muwafaka kabisa kuchukuwa hatua ambazo zikikwepwa kuchukuliwa -yaani mageuzi makubwa kufanywa.Tunapaswa kuziletas katika hali ya kimamboleo mahkama zetu za kisheria na kuhakkisha watu wanalipa kodi zao kwa wakati."

Ikiwa na makao yake nchini Tanzania,Taasisi yake ya Investment climate Facility-ushirika kati ya makampuni ya kibinafsi,mashirika ya maendeleo na serikali inalenga kuondoa vikwazo na vizingiti vya kibiashara barani Afrika.

Ikiwa imeundwa miaka 2 iliopita kutumika kwa kipżindi cha miaka 7,hadi sasa imetumia dala milioni 175 kati ya akiba yake ya dala milioni 550 kugharimia miradi kiasi cha 30 katika nchi 10 mbali mbali za Afrika gadi desemba mwaka jana.

Issa alitoa mfano huu:Unaweza kupanga mradi mzuri wa eneo maalumu la kusafirishia nje bidhaa lakini, huhakikishi linapata umeme wa kutegemea.Na ikiwa umangimeza wa kutoza kodi haupo,eneo hilo kusafirisha nje bidhaa litakupa manufaa gani ?.

Jukwaa la Uchumi la Afrika limegundua kwamba nchi zaidi na zaidi za afrika zinapiga hodi mlangoni mwa Banki Kuu ya Maendeleo ya Afrika-African Developement Bank-iliioikopesha hivi punde Botswana kitita cha dala bilioni 1.5 kuziba pengo kubwa katika bajeti yake.Kuna nchi nyengine zinazopiga hodi,lakini Rais wa Banki hiyo Donald Kaberuka alikataa kuzitaja.

Banki Kuu ya Maendeleo ya Afrika yenye makao makuu yake mjini Tunis, shabaha yake ni kupunguza hali ya umasikini barani Afrika na kuc hangia fedha kuhimiza maendeleo tangu ya uchumi hata ya kijamii.

Msukosuko wa uchumi ulimwenguni umeiathiri mno Botswana na umeteremsha bei na mahitaji ya madini yake ya almasi ambayo ndio uti wa mgongo wa nchi hii ya kusini mjwa Afrika.

Nae Katibu-mkuu wa zamani wa UM Kofi Annan, aliliambia Jukwaa hilo :

"Kuna baadhi ya mambo, viongozi wanapaswa kutenda .Tuna raslimali chache na yatupasa kuzitumia vyema.Tunakabiliwa na hatari ya kurejeshwa nyuma na Banki kuu ya Dunia imeshabainisha kuwa ,ukuaji uchumi utanguka kwa 2%-nataraji hautateremka zaidi.Lakini, wanataraji pia msaada kutoka kwa washirika wao."

Mwandishi:Ramadhan Ali/RTRE

Mhariri:M.Abdul-Rahman