1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Julien Paluku ajiuzulu ugavana Kivu Kaskazini

Grace Kabogo
25 Februari 2019

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, amekutana na kuwaomba wabunge kutoka vuguvugu lake la kisiasa la FCC kubaki katika mshikamano ili kukabiliana na changamoto za kisiasa.

https://p.dw.com/p/3E2Ff

Vuguvugu hilo lilipata ushindi wa viti 330 kati ya viti 500 na linataka lipewe nafasi ya uwaziri mkuu na kuunda baraza la mawaziri.

Mwandishi wetu, Saleh Mwanamilongo, amefanya mahojiano maalum na Julien Paluku, aliyekuwa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini ambaye hivi sasa ni mbunge na mmoja wa viongozi wa vuguvugu hilo.

Paluku ametangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake wa ugavana na kusema hatagombea tena muhula mwingine. Kwanza anaelezea lengo la mazungumzo yao na Rais Mstaafu Kabila mjini Kinshasa.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Mohammed Khelef