1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juma Ali Khatib naye ataka kumrithi Karume Zanzibar

13 Oktoba 2010

Homa ya Uchaguzi wa Oktoba 31 inazidi kupanda nchini Tanzania, na sasa hata vyama vidogo visiwani Zanzibar vinapania kumrithi Rais anayemaliza muda wake, Amani Karume, kama TADEA iliyomsimamisha Juma Khatib

https://p.dw.com/p/PCYL
Amani Karume, Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake
Amani Karume, Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wakePicha: Mohammed Khelef

Miongoni mwa vyama hivyo ni kile cha TADEA ambacho hakikuwahi kuwa na muakilishi si katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala baraza la wawakilishi huko Zanzibar. Safari hii TADEA kimemteua Katibu wake mkuu Bw Juma Ali Khatib kugombea Urais wa Zanzibar. Nimezungumza naye kwa njia ya simu na kwanza anaelezea kwanini wakachukua uamuzi huo katika uchaguzi huu wa 2010.