1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya kimataifa yalaani mapinduzi Mali

Sekione Kitojo
20 Agosti 2020

Kanali wa jeshi Assimi Goita alijitambulisha kuwa kiongozi wa kijeshi wa Mali siku moja baada ya mapinduzi nchini humo ambayo yamelaaniwa na jumuiya ya kimataifa lakini amepata uungwaji mkono kutoka upinzani nchini humo.

https://p.dw.com/p/3hEOG
Mali Assimi Goita
Kanali Assimi Goita akizungumza na waandishi habari katika mji mkuu wa Mali Bamako, 19.08.2020Picha: Getty Images/M. Konate

Umoja wa Afrika, Umoja  wa  Ulaya, Marekani  na  baraza la Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  zote zimetaka uongozi huo wa kijeshi kumwachia  huru  rais Ibrahim Boubacar Keita , waziri mkuu Boubou Cisse  na  wengine ambao wamekamatwa  katika  mapinduzi yaliyofanyika  siku  ya  Jumanne kufuatia  maandamano  ya miezi kadhaa.

Katika  mji mkuu  wa  Mali  Bamako, Goita  alisema  baada  ya kukutana  na  watendaji wakuu  wa  kiraia  kuwa yeye  ndio kiongozi wa "kamati ya  taifa kwa  ajili ya  uokozi wa  umma" ambayo imekamata madaraka.

Rücktrittserklärung von Malis Präsident Boubacar Keita auf ORTM
rais aliyeondolewa madarakani nchini Mali, Ibrahim Boubacar Keita akitoa maelezo ya yeye kuondolewa madarakani Picha: ORTM/Reuters

"Mali imo katika  hali mzozo wa  kisiasa na kijamii. Hakuna  nafasi tena ya kufanya  makosa." Goita aliwaambia waandishi  habari  huku akiwa  amezungukwa  na  wanajeshi. Umoja  wa Afrika umeshutumu kile  ilichosema  kuwa  ni  "mabadiliko ya serikali ambayo  ni kinyume  na  katiba" nchini Mali.

Kundi  hilo  la  mataifa  limetangaza  kuwa  linasimamisha uanachama  wa  Mali , ikiwa  ni  hatua  ambayo si  ya  kawida inayomzuwia  mwanachama  kuhudhuria  mikutano  yote  ya  kilele na  mikutano  ya  kawaida, "hadi pale  utaratibu wa  kikatiba utakaporejeshwa." Waziri wa mambo ya kigeni waq  Niger Kalla Ankourao  ameeleza kusikitishwa kwa jumuiya ya ECOWAS kutokana na  mapinduzi hayo

Uongozi wa kijeshi wa Mali

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesisitiza wito wake  jana wa  kurejea  katika  utawala  wa  kiraia. Nae waziri wa mambo  ya kigeni  wa  Ujerumani Heiko Maas  amesema anaungana na Ufaransa  na kundi  la  mataifa wanachama  wa  jumuiya  ya ECOWAS kuwataka wanajeshi kurejesha  uongozi wa  kiraia.

Russland: Außenminister Maas in Moskau
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko MaasPicha: picture-alliance/dpa/Russian Foreign Ministry

"Tunazungumza  na wenzetu wa Ufaransa  ili  kupata  taarifa  zaidi juu ya  kutoa usaidizi kwa madai ya jumuiya ya ECOWAS kutaka kurejesha utawala wa kikatiba. Na kutokana na tathmini yetu ni lazima mapinduzi haya yasitishwe."

Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa  Marekani  Mike Pompeo  alisema kuwa Marekani, inashutumu  vikali  uasi  wa  Agosti 8 nchini  Mali kama  tunavyoshutumu  hatua  yoyote  ya  kuchukua  madarakani kwa  nguvu."

Dominikanische Republik Pompeo bei Amteinführung Präsident Luis Abinader
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Heiko MaasPicha: Getty Images/AFP/O. Barria

Amesema  uhuru  na  usalama  wa  maafisa  wa  serikali waliokamatwa  pamoja  na  familia  zao  ni  lazima  uhakikishwe," amesema.

Mataifa 15 ya Jumuiya  ya  maendeleo  ya  Afrika  magharibi ECOWAS , ambayo  yamejaribu  bila  mafanikio  kusimamia mapatano  katika  mzozo  huo  wa kisiasa  wa  muda  mrefu , pia utasitisha  uanachama  wa  mali  katika  vyombo  vyake  vya  ndani vinavyofanya  maamuzi.