1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Maafa yaendelea kutokea Afghanistan.

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrS

Polisi wa kusini mwa Afghanistan wamesema mtu mmoja aliyekuwa akiendesha gari lililotegwa bomu, ameligonga gari la majeshi ya NATO na kusababisha vifo vya watoto watano raia wa Afghanistan, mwanajeshi mmoja kutoka Uholanzi na wanaume wanne wa Afghanistan katika mji wa Tirin Kot.

Majeshi ya NATO yamesema wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Saa chache baadaye raia watano walijeruhiwa kwenye shambulio la bomu lililotekelezwa na mtu mwengine aliyejitoa mhanga katika mji wa Kandahar kiasi kilomita mia moja kutoka Tirin Kot.