1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Miripuko yauwa wanne

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC80

Miripuko miwili tafauti katika mji wa kusini mashariki wa Afghanistan imeuwa watu wanne na kujeruhi wengine kadhaa.

Katika mji wa Khost muuaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa wakati polisi ilipokuwa ikijaribu kumzuwiya na kupelekea kuuwawa yenye mwenyewe na raia watatu.

Shambulio la awali katika soko lililojaa watu limemuuwa muuza duka mmoja.Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Hapo jana wanamgambo wa Taliban walikivamia kituo cha polisi katika jimbo jirani la Paktia na katika mapambano yaliofuatia waasi watano na polisi mmoja waliuwawa.