1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Operesheni kubwa imefanywa na majeshi ya Uingereza.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOO

Majeshi ya Uingereza nchini Afghanistan yamefanya operesheni kubwa ya kijeshi katika jimbo la kusini la Helmand. Kiasi cha wanajeshi 2 500 kutoka katika jeshi linaloongozwa na NATO walianza operesheni hiyo leo Jumatano asubuhi kuwaondoa wapiganaji wa Taliban kutoka katika bonde la mto Helmand. Majeshi ya Uingereza yanajaribu kwa taratibu kupanua udhibiti wa serikali ya Afghanistan katika miji na vijiji katika bonde hilo ambako inasemekana kuwa madawa ya kulevywa yanalimwa. Helmand pia ni jimbo ambalo linatokea matukio mengi ya ghasia kutokana na mashambulizi ya kila siku baina ya wapiganaji wa Taliban na majeshi ya Afghanistan, Uingereza na Marekani.