1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Raia wauwawa na majeshi ya Marekani.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC37

Majeshi ya NATO nchini Afghanistan yamethibitisha kuwa kumekuwa na vifo vya raia katika mapigano baina ya majeshi ya Marekani na wapiganaji wa Taliban kusini mwa nchi hiyo.

Katika taarifa jeshi la kimataifa la kulinda amani ISAF , limesema kuwa raia 20 waliojeruhiwa wamepata matibabu katika jimbo la Helmand , ikiwa ni pamoja na mtoto ambaye alifariki baadaye kutokana na majeraha.

Gavana wa jimbo la Helmand Assadullah Wafa amesema kuwa raia 22, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto wameuwawa.

Raia wa kawaida wamesema kuwa idadi ya watu waliouwawa ni kubwa.