1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulizi la bomu dhidi ya polisi limeua watu 35

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqq

Wanamgambo wa Taliban wamedai kuwa ndio waliohusika na shambulizi la bomu lililofanywa asubuhi ya leo katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.Bomu liliripuka ndani ya basi mbele ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul.Kwa mujibu wa maafisa,basi hilo lilikuwa likiwapeleka walimu kwenye taasisi ya polisi.Baadhi kubwa ya wale waliouwa walikuwa maafisa wa polisi.Miongoni mwa watu waliofariki ni Wajapani 2,raia mmoja wa Korea ya Kusini na Wapakistani 2.Wageni hao lakini walikuwa katika basi jingine lililokuwa likipita karibu na eneo hilo,mripuko huo ulipotokea.Wafanyakazi hao wa kigeni walikuwa wakilifanyia kazi shirika linalowapatia makazi na elimu watoto wasio na makwao katika mji wa Kabul.Hilo ni shambulizi baya kabisa kutokea nchini Afghanistan,tangu serikali ya Wataliban kutimuliwa mwaka 2001.