1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wataliban wateka mji kusini mwa Afghanistan

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVR

Mamia ya wanamgambo wa Kitaliban wameuteka mji wa Musa Qala kusini mwa Afghanistan.Mwaka jana, baada ya kupatikana makubaliano ya amani,vikosi vya Kingereza viliwakabidhi wakuu wa kikabila mji huo.Ripoti zinasema,wanamgambo wa Taliban wameteka silaha kutoka kituo cha polisi mjini Musa Qala na wameteketeza jengo la Halmashauri ya Mji katika wilaya ya Helmand.Inasemekana kuwa wakazi katika eneo hilo wanauhama mji,wakiwa na hofu kuwa wanamgambo wa Kitaliban watashambuliwa kutoka angani na vikosi vya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi-NATO.Maafisa wa NATO wanasema,wanaamini kuwa vikosi vya Taliban viliuvamia mji huo kulipiza kisasi shambulio la angani liliofanywa na NATO juma lililopita.Ndugu wa kamanda mmoja wa Taliban aliuawa katika shambulio hilo.