1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:14 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Afghanistan

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC06

Watu 14 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katikati ya kundi la watu huko kusini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Mashuhuda wamesema kuwa mtu huyo alijilipua kwenye soko lililokuwa na watu wengi kwenye eneo la Gardez lililoko katika jimbo la Paktia.

Wanamgambo wa Taliban wamedai kuhusika na shambulizi hilo, ambalo lilitokea wakati majeshi ya NATO yalipokuwa yakipita kwenye eneo hilo.

Baadhi ya taarifa zinadai kuwa miongoni mwa majeruhi ni askari wa jeshi hilo la washirika.

Shambulizi hilo la jana ni la pili katika muda wa siku mbili kutokea huko Afghanistan.Hapo siku ya Jumamosi watu tisa waliauawa wakiwemo askari watatu wa Ujerumani na wengine wanne kujeruhiwa.

Askari waliyojeruhiwa wamerejeshwa hapa Ujerumani mjini Koln kwa matibabu.

Wakati huo huo, Majeshi ya NATO na yale ya Afghanistan yamesema kuwa yamewaua watu 30 wanaohisiwa kuwa wapiganaji wa kitaliban wakati wa mashambulizi ya alfajiri leo huko katika jimbo la kusini la Ghazni.