1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Wateka nyara wasema mazungumzo yamefikia mahali muhimu

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfY

Wanamgambo wa Taliban wamesema kuwa mazungumzo juu ya majaaliwa ya mateka 23 raia wa Korea Kusini inaowashikilia nchini Afghanistan yamefikia katika hatua muhimu baada ya muda wa mwisho waliyouweka kupita hapo jana.

Wanamgambo hao wanataka kuachiwa kwa wenzao wanaoshikiliwa katika magereza nchini Afghanistan.

Wakati huo huo mateka mwengine raia wa Ujerumani ambaye pia anashikiliwa na wataleban,inasemekana anaumwa na yuko katika hali mbaya kutokana na kukosa matibabu.

Mwili wa mateka mwengine wa Ujerumani unatarajiwa kuwasili hapa nchini hii leo.Mwili wake ulikutwa na majeraha ya risasi.

Mapema wanamgambo hao wakitaleban walitoa madai ya kuzitaka Ujerumani na Korea Kusini kuondoa majejshi yao nchini Afghanistan kama shatri la kuachiwa kwa mateka hao.