1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: LRA-Makubaliano kuweka chini silaha hayatorefushwa

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOz

Kundi la waasi la Uganda-LRA limesema halitorefusha makubaliano pamoja na serikali kuweka chini silaha,ambayo muda wake unamalizika juma lijalo.Naibu kamanda wa LRA,Vincent Otti ameituhumu serikali kuwa inakwenda kinyume na makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.Hapo awali,msemaji wa jeshi la Uganda Meja Felix Kulaije alisema,serikali ipo tayari kurefusha makubaliano ya kuweka chini silaha,ikiwa waasi watakwenda Juba,kusini mwa Sudan,kutia saini makubaliano hayo.